Machozi ya furaha Farouk Kibet akigharamia Sh2m za upasuaji wa mama Khasoa India
Hatua ya Farouk ‘Akhonya’ Kibet kuingilia kati na kumlipia gharama ya matibabu ya mama mmoja kutoka kijiji Matioli wadi ya Butali/Chegulo eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega imekaribishwa kwa furaha kubwa na wenyeji.

Familia ya Jeniffer Khasoa Barasa sasa sasa ina kila sababu ya kutabasamu baada yake kupata ufadhili wa zaidi ya shillingi million mbili nukta tatu ili kumwezesha kusafiri hadi India kufanyiwa upasuaji kwenye mguu wake wa kulia ambao umeugua kwa muda mrefu.
Kibet pia alifanikisha kupatika kwa vyeti vya usafiri na nauli ya ndege.
Viongozi wa kisiasa wametakiwa kuiga mfano huo bali sio kusaidia wakati ambapo wanatafuta kupigiwa kura.
Familia hiyo sasa itaanda ibaada maalumu jumapili hii ya tarehe 19 mwezi wa April kabla yake kusafiri na miongoni mwa watakaohudhuria ni diwani wa eneo hilo Kevin Mahelo na Mbunge wa Malava David Ndakwa.





